Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akifafanua jambo
wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge alipozungumza na
wadau wa usafishaji katika Stendi Kuu ya muda ya Mabasi ya Mikoani
iliyopo eneo la Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi
katika stendi hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na wadau wa
usafishaji katika Stendi Kuu ya muda Mabasi ya Mikoani iliyopo eneo la
Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi katika stendi hiyo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (katikati)
akifafanua jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge
(kushoto) alipofanya ziara fupi kukagua maeneo yanayoweza kuwekewa
miundombinu muhimu na kutumika kama kituo cha daladala cha Mjini, jana
Aprili 3, 2018. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Ludigija
Ndwata.
Na Ramadhani Juma,Ofisi ya Mkurugenzi
MKUU
wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameelekeza matumizi ya
kilichokuwa kituo Kikuu cha Mabasi madogo maarufu kama Daladala cha
Jamatini Mjini Dodoma kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria wanaotoka
katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo yaendelee kama kawaida wakati
Manispaa ikiandaa eneo mbadala.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia ameagiza ‘ruti’ za Daladala zifupishwe kama ilivyokuwa
awali, na kwamba upangaji wa ‘ruti’ ndefu ujadiliwe upya na wadau wote
wanaohusika na endapo utakubaliwa na wengi ndipo utekelezaji wake uanze.
Dokta
Mahenge ametoa maelekezo hayo leo Aprili 3, 2018, alipokuwa akizungumza
na wadau wa usafirishaji katika kituo kikuu cha mabasi ya Mikoani cha
muda kilichopo Nanenane Manispaa ya Dodoma baada ya kituo hicho kufungwa
wiki iliyopita kwa ajili ya kupisha mradi wa Reli ya Kisasa.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya majadiliano na wadau wote ikiwemo Mamlaka ya
Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMTRA), Manispaa, Jeshi la
Polisi, na Shirika la Reli ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, na kwamba
matumizi ya stendi hiyo yataendelea kwa muda wa miezi miwili kuanzia
sasa, kipindi ambacho Manispaa itatakiwa kuwa imeshapata na kuandaa
stendi mbadala.
Akizungumza
katika eneo la tukio, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
Godwin Kunambi alisema Manispaa imepokea maagizo yote na itahakikisha
inaandaa eneo kwa ajili ya Stendi ya Mabasi madogo Mjini katika kipindi
cha miezi miwili kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa.
Katika
hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza mabasi yote yanayosafirisha
abiria Mikoa mbalimbali Nchini kupakia na kuanzia safari zao katika
kituo Kikuu cha mabasi ya muda kilichopo Nanenane na Kampuni
itakayokiuka itachukuliwa hatua kali za Kisheria.
“Namuagiza
Mkuu wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa kuwa,
kuanzia kesho mabasi yote yauze tiketi na kuanza safari zao hapa katika
kituo hiki Kikuu cha mabasi cha muda cha Nanenane…hakuna Mkubwa wala
mdogo katika kutoa huduma kwa Wananchi” alisisitiza Dkt. Mahenge.
0 comments:
Post a Comment