Mwonekano wa moja ya mabweni Shule ya Wasichana Kondoa baada ya Ukarabati
Mwonekano wa moja ya mabweni Shule ya Wasichana Kondoa kabla ya ukarabati
Ukarabati
wa shule ya Wasichana ya Kondoa umeanza kuleta nuru ambayo uongozi na
walimu wa shule hiyo waliitamani kwa kipindi kirefu baada ya baadhi ya
mabweni kuanza kukamilika.
Akiongea
ofisini kwake Makamu Mkuu wa Shule Mwalimu Khalifa Kinasha alisema kuwa
mabweni yaliyokamilika yameanza kuonekana vizuri jambo ambalo walikuwa
wakilitamani kwa kipindi kirefu.
Aliongeza
kuwa kamati ya shule ya ujenzi inaendelea vizuri na majukumu yake ili
kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango
vinavyotakiwa ili mwonekano wa shule uwe mzuri kwa ajili ya kuhakikisha
wanafunzi wanajifunzia sehemu nzuri na walimu wanafundishia mazingira
yanayovutia.
“Kwa
kweli tunaishukuru sana serikali ya awamu ya tano wametuona kwa wakati
muafaka kwani ukarabati huu umetufanya tuone serikali inatujali na ipo
pamoja na sisi na tunaahaidi kuwa kwasasa tutafanya kazi na kupandisha
ufaulu maradufu.”Alisema Kinasha
Mhandisi
Mshauri wa mradi kwa upande wake alisema kuwa kazi inaendelea vizuri na
wameongeza nguvu ya mafundi ili kuhakikisha kuwa kazi inakamilika kwa
wakati kama ilivyopangwa kwani hakuna tatizo lolote kubwa linalowakabili
kwasasa.
“Hadi
sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 40 ambapo mabweni na baadhi ya
madarasa yamekamilika na mengine yanaendelea na ukamilishaji bwalo la
chakula linaendelea na ukarabati ikiwa ni pamoja na vyoo ambavyo baadhi
vimekamilika na vingine bado.”Alisema Mzava
Ukarabati
wa shule ya Wasichana Kondoa ulianza mapema mwezi Februari 2018 na
unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei 2018 ikiwa ni shule mojawapo
kati ya shule kumi kongwe zinazokarabatiwa na serikali kwa awamu ya
kwanza na ilipewa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja.
0 comments:
Post a Comment