Home » » MAENEO YENYE MIGOGORO NA HIFADHI KUFANYIWA TATHMINI.

MAENEO YENYE MIGOGORO NA HIFADHI KUFANYIWA TATHMINI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Maeneo yote yenye mgogoro kati ya wananchi na hifadhi za taifa yatafanyiwa tathmini ili kuondoa migogoro iliyopo.
 
Hayo yalisemwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Felista Bura, aliyetaka kujua ni lini mgogoro kati ya wananchi na hifadhi ya Mkongonero utamalizwa na serikali. 
 
Prof. Maghembe alisema mpango huo umeandaliwa na wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 
Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Cecilia Pareso,  alitaka kujua matokeo ya kamati ndogo iliyoundwa na waziri wa maliasili na utalii aliyepita kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wananchi wa kata ya Buger na Hifadhi ya Taifa ya Manyara.
 
Akijibu, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ramo Makani, alisema kamati hiyo ilibaini chanzo kikubwa cha migogoro baina ya wananchi na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ni idadi kubwa ya mifugo na kukosekana eneo la kuchungia katika kijiji cha Buger.
 
Alitaja miongoni mwa hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kuwa ni, kufanya sensa ya mifugo kwa vijiji vilivyopo katika kata hiyo ili kubaini idadi ya mifugo iliyopo dhidi ya ukubwa wa ardhi waliyonayo.
 
Nyingine ni vijiji kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi, kutoa elimu ya uhifadhi na sheria katika vijini na kuimarisha zilizopo ili kutelekeza vema majukumu yake.
 
Aidha, alisema  hatua nyingine ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) kuchangia miradi ya maendeleo ya jamii kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa