Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Maeneo yote yenye mgogoro kati ya wananchi na hifadhi za taifa yatafanyiwa tathmini ili kuondoa migogoro iliyopo.
Hayo yalisemwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, wakati akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Felista Bura, aliyetaka kujua ni lini
mgogoro kati ya wananchi na hifadhi ya Mkongonero utamalizwa na
serikali.
Prof. Maghembe alisema mpango huo umeandaliwa na wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema),
Cecilia Pareso, alitaka kujua matokeo ya kamati ndogo iliyoundwa na
waziri wa maliasili na utalii aliyepita kushughulikia mgogoro uliopo
kati ya wananchi wa kata ya Buger na Hifadhi ya Taifa ya Manyara.
Akijibu, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ramo Makani, alisema kamati
hiyo ilibaini chanzo kikubwa cha migogoro baina ya wananchi na Hifadhi
ya Taifa ya Ziwa Manyara ni idadi kubwa ya mifugo na kukosekana eneo la
kuchungia katika kijiji cha Buger.
Alitaja miongoni mwa hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kuwa ni,
kufanya sensa ya mifugo kwa vijiji vilivyopo katika kata hiyo ili
kubaini idadi ya mifugo iliyopo dhidi ya ukubwa wa ardhi waliyonayo.
Nyingine ni vijiji kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi, kutoa
elimu ya uhifadhi na sheria katika vijini na kuimarisha zilizopo ili
kutelekeza vema majukumu yake.
Aidha, alisema hatua nyingine ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
(Tanapa) kuchangia miradi ya maendeleo ya jamii kwenye vijiji
vinavyozunguka hifadhi.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment