Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama
Serikali imeanza kurejesha kwa haraka mawasiliano ya
barabara yaliyokatika kati ya wilaya za Kilombero na Ulanga, mkoani
Morogoro kutokana na mvua zilizonyesha na kusababisha kivuko cha mto
Kilombero kuzama.
Akizungumza wakati akitoa taarifa ya awali ya serikali kuhusiana na
tukio hilo bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (pichani), alisema sasa
timu za kazi za kiutendaji zipo kazini kuangalia namna ya kulishirikisha
jeshi katika kazi hiyo.
Alisema serikali ilipata taarifa ya awali juu ya tukio hilo usiku
wa kuamkia jana na kwamba kivuko hicho kilikuwa kimebeba abiria 31,
magari matatu na bajaj mbili na mpaka jana kwa taarifa walizokuwa nazo,
abiria 30 wameshaokolewa.
Mhagama aliwasihi wananchi kutulia kwa kuwa serikali tangu
ilipopokea taarifa hiyo imekuwa ikishughulikia haraka ili kuona nini
kifanyike na kwa wakati gani.
Alitoa wito kwa Watanzania kuchukua tahadhari ya mvua zinazoendelea kunyesha, kwani kwa mujibu wa watabiri wa hali ya hewa, mvua nyingi na upepo mkalai na dhoruba vinatarajiwa kutokea.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment