Home » » NDUGAI KUTANGAZA KAMATI ZA BUNGE LEO

NDUGAI KUTANGAZA KAMATI ZA BUNGE LEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo atatengua kitendaliwi cha kamati za Bunge kwa kutangaza wajumbe wake na zitaanza vikao vyake leo mjini Dodoma.
 
Kamati hizo ni ya uongozi, Kamati ya Kanuni za Bunge, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Nishati na Madini, Kamati ya Bajeti, Kamati ya Masuala ya Ukimwi, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana kuhusu ratiba ya semina ya  wabunge wote pamoja na vikao vya kamati za kudumu za Bunge vitakavyofanyika mjini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Bunge, Owen Mwandumbya, alisema Spika Ndugai atatangaza kamati hizo leo na kuanza vikao vyake mara moja.
 
Alisema vikao hivyo vitaanza leo saa 4:00  asubuhi kwa kufanya uchaguzi wa wenyeviti wake na makamu wao.
 
Aidha, katika semina ya wabunge wote itakayofanyika leo, wataelezwa wajibu, kazi na mipaka ya kazi za kamati na kupokea na kujadili mpango kazi wa kamati unaoishia Juni, 2016.
 
Mkutano wa pili wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza Januari 26, mwaka huu mjini hapa.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa