Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo atatengua
kitendaliwi cha kamati za Bunge kwa kutangaza wajumbe wake na zitaanza
vikao vyake leo mjini Dodoma.
Kamati hizo ni ya uongozi, Kamati ya Kanuni za Bunge, Kamati ya
Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati
ya Kilimo, Mifugo na Maji, Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Nishati na
Madini, Kamati ya Bajeti, Kamati ya Masuala ya Ukimwi, Kamati ya Hesabu
za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana kuhusu ratiba ya
semina ya wabunge wote pamoja na vikao vya kamati za kudumu za Bunge
vitakavyofanyika mjini Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Bunge, Owen Mwandumbya, alisema Spika Ndugai atatangaza kamati hizo leo
na kuanza vikao vyake mara moja.
Alisema vikao hivyo vitaanza leo saa 4:00 asubuhi kwa kufanya uchaguzi wa wenyeviti wake na makamu wao.
Aidha, katika semina ya wabunge wote itakayofanyika leo, wataelezwa
wajibu, kazi na mipaka ya kazi za kamati na kupokea na kujadili mpango
kazi wa kamati unaoishia Juni, 2016.
Mkutano wa pili wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza Januari 26, mwaka huu mjini hapa.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment