Home » » WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAHAKIKI WASTAAFU MKOANI DODOMA

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAHAKIKI WASTAAFU MKOANI DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.



Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Wizara ya Fedha na Mipango, imezindua zoezi la uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara hiyo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma mkoani Dodoma.
 Lengo la kufanyika kwa zoezi hili ni kuhuisha orodha ya malipo ya Wastaafu kwa mara ya mwisho zoezi hilo lilifanyika mwaka 2014.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Stanslaus Mpembe, alisema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku tano katika Kanda ya Kati ambayo imejumuisha mikoa mitatu ya  Morogoro, Dodoma na Singida.
Mpembe alisema lengo la kufanyika kwa zoezi hilo ni kubaini mabadiliko ya taarifa za Wastaafu kama vile kufariki ili kuepuka kulipa Wasiostahili.
‘Zoezi hili linafanyika kutokana na utaratibu uliojiwekea Wizara kufanya uhakiki wa Wastaafu baada ya muda fulani, zoezi hili litafanyika nchi nzima. Mpembe alisema’
Aliongeza kuwa zoezi hilo litaisaidia Serikali kuhakikisha Wastaafu wote wanapata haki zao na kwa wakati.
Aidha alitoa wito kwa Wastaafu kujitokeza kwa wingi kuhakikiwa ili waweze kupata haki zao za msingi, bila kusahau viambatanisho wanavyotakiwa kuwa navyo ili kurahisisha zoezi hilo.
Naye Katibu wa Chama Cha Wastaafu wa Mkoa wa Dodoma John Kanyeto aliishukuru Serikali kwa kuwajali na kukubali ombi lao kuhusani Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji  kwa kufikisha ombi lao walipofanya nae kikao la kulipwa mafao yao kila mwezi badala ya kila baada ya miezi mitatu.
‘Niwaombe Wastaafu wenzangu wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hilo ni la kwa faida yao. Kanyeto aliongeza’.
Kwa upande wa mstaafu Bi. Halima Matonya alisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na ameipongeza Serikali kwa kuwajali na kuwakumbuka, na amewapongeza  pia Waratibu wa zoezi hilo kwa kujipanga vema na kutoa maelekezo vizuri hivyo kufanya zoezi hilo kuchukua muda mchache.
Tayari zoezi kama hilo la uhakiki wa wastaafumwanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango limefanyika katika Kanda za Pwani na Nyanda za Juu Kusini ambapo ilijumlisha mkoa wa Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Katavi, Ruvuma, na Songwe.
Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo kanda ya kati, zoezi hilo litaendelea katika Kanda ya Kaskazini ambapo litajumuisha Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga.

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa