Masoud Masasi,Kondoa -Dodoma Yetu
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umesema unaupungufu wa damu wa chupa
350,000 katika benki zake zilizopo hapa nchini jambo ambalo wamesema
likifanya kushindwa kusambaza damu ya kutosha katika hospitali
mbalimbali.
Hali hiyo imeelezwa inatokana na wananchi kutokuwa na mwamko wa
uchangiaji wa damu pindi wanapotakiwa kuchangia badala yake wanafunzi
ndio wamekuwa wakijitolea kutoa damu.
Hayo yalibainishwa juzi wilayani hapa na Meneja wa Mpango wa Damu
Salama kanda ya Mashariki Grace Mlingi wakati wa maadhimisho ya siku
ya wachangiaji damu duniani.
Mlingi alisema hatua hiyo ya kutokuwa na damu ya kutosha hapa nchini
inatokana na kutokuwa na mbadala wa upatikaji wa damu salamuisipokuwa
kutoka kwa binadamu.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakishindwa kujitokeza kwenye sehemu
ya utoleaji damu zaidi ya kuwapata wanafunzi peke yake jambo alilosema
halipendezi kwa kuwa damu hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya watu wote.
‘’Tunaupungufu mkubwa wa chupa za damu kwenye benki zetu hapa nchini
nah ii inatokana na kutokuwa na mwamko kwa wananchi licha ya jitihada
mbalimbali za kutoa elimu lakini bado mkitangaza wanakuja wanafunzi
pekee”alisema Mlingi.
Meneja huyo alibainisha kuwa kuchangia damu kunasaidia kuepusha vifo
kwa watoto wadogo,wajawazito pamoja na majeruhi ambao wamekuwa
wakihitaji damu kutokana na kuishiwa hivyo kuwepo kwa damu za kutosha
kutachangia kuepukana na tatizo hilo.
Akizungumzia mahitaji ya damu katika kanda ya Mashariki,Mlingi alisema
wanahitaji chupa za damu 80,000 sawa na asilimia 67 ili ziweze
kukidhi mahitaji ya kanda hiyo.
“Mahitaji haya tunaweza kufanikiwa ikiwa wananchi watajitokeza
kuchangia damu katika kanda yetu ili tuweze kukabiliana na upungufu
huo inabidi tujitokeze kutoa damu tusiogope”alisema meneja huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Umma na Uhamasishaji wa mpango huo
katika kanda hiyo Lucas Michael alisema bado elimu kubwa inahitaji
kwa wananchi juu ya suala nzima la uchangiaji wa damu salama.
Alisema wananchi wamekuwa na imani potofu kuwa ukitoa damu unaweza
kupoteza maisha huku wengine wakiohofu kuwa watapimwa ukimwi kabla ya
kutoa damu.
“Kabla ya kuanza kutoa damu vitu ambavyo anapimwa mtoaji damu ni
uzito,kiwango cha damu na msukumo wa damu pekee ambapo baadaye baada
ya kukusanywa ndipo zinapimwa virusi vya ukimwi,homa ya ini na
kaswende ”alisema Michael.
Hata hivyo katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kikanda wanafunzi wa
shule ya sekondari ya wasichana ya Kondoa ndio pekee walioweza
kujitolea kuchangia damu.
0 comments:
Post a Comment