Home » » wanawake msiwashawishi kwa rushwa ya ngono mainjinia

wanawake msiwashawishi kwa rushwa ya ngono mainjinia

Masoud Masasi, Dodoma

WANAWAKE wakandarasi hapa nchini wametakiwa kuwa waaminifu katika kujaza kabrasha la zabuni(Tender Document) na kusoma mikataba vizuri  kabla ya kuijaza, ili kuondoa migogoro na lawama na rushwa za ngono zinazotolewa kwa mainjinia ambao ndio wakaguzi wa makabrsaha hayo.

Wito huo ulitolewa mjini hapa jana na mwenyekiti wa taifa wa bodi ya wakandarasi Consolata Mgimbwa, wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya kuwajengea wanawake, uwezo wa kujenga na kutengeneza barabara kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi.

Alisema kuwa kumekuwepo na tatizo kubwa katika ujazaji wa makabrasha  hayo kitendo ambacho kimekuwa kikisababisha migogoro kwa mainjinia ambao ndio wanaozikagua na kuzipisha zabuni hizo.

Mgimbwa alisema Mainjinia wamekuwa wakilaumiwa sana na kuonekana wanafanya upendeleo katika upitishaji wa tenda za makandarasi kumbe makandarasi wenyewe ndio wanaokosea kujaza kabrasha za zabuni na kusababisha washindwe kutozipitisha.

“Hata kama ingekuwa mimi siwezi kuahangaika na mtu ambaye amejaza taarifa zake za zabuni vibaya wakati kuna mtu amejaza vizuri na zinaeleweka nampitisha tu huyo” alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha aliwataka wanawake kuacha kuwatia majaribuni mainjia kwa kuwatongoza ili waweze kuwapitishia tenda zao na badala yake wajiamini na kufanya vitu vizuri ili viweze kujipitisha vyenyewe bila vishawishi vya rushwa ya ngono.

“Yani inashangaza sana utaona mwanamke anamuita injinia nyumbani kwake na kuanza kumtongoza ili ampitishie teda matokeo yake na yulemwanaume analubunika kwa kuwa yeye ni binadamu anajikuta anaingia katika rushwa ya ngono”

“ jamani chema kinajiuza mi naamini tukijaza taarifa zetu vizuri zitapita tu”Alisisitiza Mgimbwa.

Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwaasa wanawake kutokuwa waogo na kujiunga katika vikundi ili waweze kupata kazi za ujenzi wa barabara kwa urahisi kuliko wakiwa mmoja mmoja.

Alisema wizara kupitia kitengo cha ushirikishwaji wa wanawake iliona umuhimu wa wanawake kuingia katika kazi za ukandarasi na ndio mana imeamua kuanzisha mafunzo haya ambayo yatawashirikisha kikamilifu wanawake kaika nchi nzima.

Alisema mafunzo hayo yatasaidia kuongeza idadi ya makandarasi wanawake kutoka 1000 waliopo hivi sasa ambao ni kati ya wanaume 6000 waliopo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa