Home » » MED YATOA VITABU VYA MIL. 300/-

MED YATOA VITABU VYA MIL. 300/-

na Danson Kaijage, Chamwino
ASASI ya kiraia ya Marafiki wa Elimu mkoani Dodoma (MED) kupitia maradi wake wa ‘haki yangu, sauti yangu,’ imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni 300.9 kwa shule 82 msingi na sekondari  za wilayani Chamwino.
Akizunguza wakati wa kuutambulisha maradi huo kwa mkuu wa wilaya hiyo, mratibu  wa mradi, Davis Makundi, alisema kuwa lengo lao ni kusaidia kukuza kiwango cha elimu wilayani humo na kuwajengea uwezo wanafunzi.
Makundi alisema jumla ya shule hizo 82 zimepatiwa vitabu vya kiada kwa ajili ya masomo ya Hesabu, Kiingereza na Jiografia ambavyo vitawasaidia wanafunzi kujifunza kwa wepesi zaidi kuliko ilivyokuwa awali.
Alisema kuwa asasi hiyo imevinunua vitabu hivyo kupia fedha za ufadhili zilizotolewa na Shirika la Oxfarm GB na halmashauri hiyo imegharamia katika kuvisambaza shuleni .
Aliongeza kuwa mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Oxfarm Gb na utaendeshwa kwa kipindi cha miezi sita, ambapo awamu ya kwanza imeanza tangu Juni mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Desemba 2012.
“Na kwa kuanzia katika suala la elimu tumetoa jumla ya vitabu 65,000 vyenye thamani ya sh 3,970,000 vya kiada kwenye shule za msingi sita na sekondari nne, ili kwanza wanafunzi wawe na vitendea kazi wakati wa kutoa elimu inayohusiana na masuala ya utawala bora na demokrasia,” alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatma Ally, aliipongeza asasi hiyo kwa kuichagua wilaya yake na kutoa angalizo kuwa masuala ya kisiasa yasiingizwe katika mradi huo.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa