Masoud Masasi, Dodoma Yetu
BONANZA la mchezo wa soka na mpira wa pete uliozikutanisha timu za maveterani kutoka mikoa minne limemalizika juzi mjini hapa kwa timu ya mkoa wa Mtwara kuibuka washindi kwa upande wa soka huku Morogoro wakiambulia pointi moja.
Bonanza hilo lililokutanisha mikoa minne ya Dodoma,Mwanza,Morogoro na Mtwara katika mchezo wa soka na mpira wa pete lilifana huku wakishiriki wakilalamikia kutokuwepo kwa zawadi yoyote kutoka kwa wadhamini ambao ni kampuni ya bia(TBL)kutotoa chochote.
Katika mchezo wa asubuhi kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Mwanza iliwachapa 1-0 timu ya Mtwara huku Dodoma wakiliza majirani zao Morogoro kwa goli 2-0 magoli yaliyopachikwa na mshambuliaji wa zamani wa timu ya Polisi Dodoma Wiston Wanjara.
Mechi za jioni Mtwara ikaichapa Dodoma kwa 2-1 ambapo goli la Mtwara limefungwa na Nicholaus Edwin huku la Dodoma likiwekwa kimiani na Mkanda Sihiana.
Kwa upande wa mpira wa pete mchezo wa mchana Dodoma ikawafunga Mwanza kwa goli 26-11,Tamisemi ikiwachapa Morogoro kwa 27-7 Mchezo wa jioni timu ya Dodoma ikifungwa na Tamisemi kwa goli 30-14 huku timu ya Morogoro ikiingia mitini kupambana na Dodoma.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment