Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakhia Megji akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mama Salma Kikwete katika ukumbi wa NEC, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu Dodoma leo, 26 Agosti 2013.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa za misiba iliyojiri, kabla ya kikao akijaanza cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea mjumbe mwenzao aliyefariki ndugu Meja Jenerali Haji Makame Rashid.
CCM YAZIDI KUWA IMARA ZAIDI
Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimemalizika jioni ya leo huku kukiwa na mabadiliko mbali mbali makubwa kwenye chama hicho.
Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa Jakaya Mrisho Kikwete kimemalizika kukiwa na mabadiliko na mapendekezo mbali mbali, kikao hicho ambacho kimekaa kwa siku tatu mfululizo kikitumia siku mbili nzika kujadili Rasimu ya Katiba na maoni ya wana CCM .
Halmashauri hiyo pia imeridhia uamuzi wa kufukuzwa uanachama Mansour Yussuf Himid kwa tuhuma za Kushindwa kusimamia malengo na madhumuni ya chama na kutekeleza masharti ya uanachama, kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka maadili ya Kiongozi wa CCM,Kuikana Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010-2015 na kukisaliti chama.
Mansour alianza uanachama tarehe 7/4/1988 na ni mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,wilaya ya Damani,Mkoa wa Magharibi Unguja.
katika hatua nyingine ya Kimaadili sula la madiwani wa Bukoba bado halijafikiwa uamuzi ingawa Kamati Kuu itakaa tena kesho tarehe 27 Agosti 2013 kufanya maamuzi ya suala la Bukoba.
Kamati Kuu pia imependekeza majina ya Makatibu wa Jumuiya,Ikiwemo Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi, Umoja wa Vijana CCM Ndugu Sixtus Mapunda, Wazazi Seif Shaaban Mohamed .
Makatibu wapya wa Mikoa walioteuliwa ni Romuli Rojas John, Kaskazini Pemba Kassim Mabrouk Mbarak na Geita Mary Maziku.
0 comments:
Post a Comment