Abiria
wakiwa tayali wameshuka katika Daladala baada ya kutoka maeneo
mbalimbali ya mji wa Dodoma na kushushiwa Barabarani baada ya kukuta
msongamano mkubwa katika stand mpya iliyoanza kutumika leo ya jamatini.
Mmoja wa viongozi wa
wafanyabiashara Ndogondogo Danny Msitewa akifafanua jambo alipokuwa
akisoma majina na kuwapa namba za utamburisho wa nafasi za kuweka
vibanda vyao katika stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma
Wafanya biashara waliokuwa stend
iliyokuwa ya muda ya daladala oil com wakikusanya bidhaa zao
zilizosambazwa na tingatinga lililofika kubomoa vibanda walivyokuwa
wakaifaanyia biashara zao ili kuwashinikiza kuondoka eneo hilo.
Asikari akitoa maelekezo kwa
baadhi ya watu waliokuwa wakivizia kukwapua mali za watu zilizozagaa
stand ya Daladala ya oil com Baada ya kubomolewa vibanda vyao ili wahame
katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Mipango miji na Mazingira manispaa ya Dodoma Stephen Mwanga akiwatangazia wafanya biashara ndogondpgo kutoendelea na ujenzi mpaka baazi ya taratibu zitakapokamilishwa. Msukuma Tololi akiingiza moja ya vibanda vya wafanyabiashara katika Stand mpya ya Daladala ya Jamatini Dodoma iliyoanza kutumika leo
Magali ya Daladala yakisubili abiria ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
Na John Banda, Dodoma
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika ugawaji.
WAKAZI wa manispaa ya Dodoma wamelalamikia udogo wa Stand kuu ya Daladala ya Jamatini na kuitaka mamlaka nayohusika kuliacha eneo la oil com zilikokuwa zikipakilia abiria wakati wa ujenzi wa stand hiyo kuwa mbadala kutokana na wingi
wa magari.
Katibu wa Umoja wa wenye Daladala [UWEDO] Peter Kabome alisema Stendi hiyo haijawa Rasmi ni kama inafanyiwa majaribio kwa sababu haiwezekanai yakatakiwa kuingizwa magali zaidi ya 300 kwenye eneo linalochukua magali yasiyozidi 100.

Daladala
zikisubili kuingia ndani ya Stand Mpya ya Jamtini Dodoma iliyoaanza
kutumia leo huku kukiwa nachangamoto ya wingi wa magali hayo kiasi cha
kushia abiria barabarani kutokana na ufinyu wa stand hiyo.
Kazi ya bomoa bomoa ikiendelea stend ya mkoa
MWENYEKITI wa kamati ya Mipango
miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi
wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya
Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.
Machinga hao wamesimamishwa
kujenga siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya
kufungwa mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya
watumiaji
wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.
wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.
Mwenyekiti huyo aliwataka
kusimamisha zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana
na kile alichosema ugawaji ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu
kutokana na viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.
Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo
hilo kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia
kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi wao
walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi huo
haujaanza Augost 2012.
Alisema alipofika na kujionea
kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali
halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda
lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa manispaa
ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.
'' Nimesimamisha ujezi usiendelee
kwa sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu
ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa
manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga
kwa upande wao baadhi ya Machinga
hao walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia
majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa hata
wakati staend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi hizo
zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika ugawaji.
TATIZO LA UDOGO WA STEND LAIBUKA
WAKAZI wa manispaa ya Dodoma wamelalamikia udogo wa Stand kuu ya Daladala ya Jamatini na kuitaka mamlaka nayohusika kuliacha eneo la oil com zilikokuwa zikipakilia abiria wakati wa ujenzi wa stand hiyo kuwa mbadala kutokana na wingi
wa magari.
Kauli hiyo ilitolewa wakati stendi
hiyo ilipoanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza jana ambapo ilishuhudiwa
wingi wa magali hayo ya Abaria yakiingia na kutoka huku kukiwa na
msongamano mkuwa kiasi cha mengine kushushia abiria Barabarani.
Mmoja wa Abiria wanaotumia stand
hiyo Winnie Binamu alisema imejengwa vizuri lakini haikidhi haja
kutokana na kuwa ndogo ukilinganisha na idadi kubwa ya Daladala zilizopo
hali inayosababisha msongamano na wengi kushusha abiria bila
utaratibu ilimradi wawahi kupakia wengine.
Winnie aliongeza kuwa niafadhali
kama wahusika wangeiacha stand iliyokuwa ikitumika kwa muda ya oili com
kuendelea kutumiwa na baadhi ya magali ya njia nyingine na mengine
kupelekwa jamatini kwa sababu kwa sasa watu ni wengi tofauti na miaka
ya nyuma.
Kwa upande wao madereva wa
Daladala hizi walisema stand pamoja na uzuri haikidha kutokana na njia
moja kuwa na magali zaidi ya 50 wakitolea mfano njia ya Chang'ombe,
Mipango, UDOM, na kisasa zenye abiria na Magali Mengi.
Mmoja wa madereva wa Daladala
zinazoelekea Ipagala Moses Mamba alisema kwa sasa Dodoma inawatu Wengi
walioletelezwa na vyuo pamaja na taasisi zilizo na zisizo za kiserekali
zinazoendelea kuhamia mkoani hapa hivyo ni vyema swala la stand hiyo
kuangaliwa upya na ikibidi iwekwe ya ziada.
'' Ona ndugu mwandishi leo ni siku
ya kwanza stand hii kuanza kutumika lakini msongamano ni kama unavyoona
wengi wanashushia abaria barabarani kuanzia hapa yanapoingilia maka
karibu na kipita shoto[ Round About] cha stand ya mabasi ya mkoani je
wakija wote kutokana na tunavyojua itakuwaje?'', Alihoji Mamba
Katibu wa Umoja wa wenye Daladala [UWEDO] Peter Kabome alisema Stendi hiyo haijawa Rasmi ni kama inafanyiwa majaribio kwa sababu haiwezekanai yakatakiwa kuingizwa magali zaidi ya 300 kwenye eneo linalochukua magali yasiyozidi 100.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya
Mipango iji na Mazingira manispaa Stephen Mwanga alisema ameona
msongamano huo jinsi ulivyo mkubwa hivyo atahakikisha anavihusisha
vyombo vinavyohusika kikiwemo SAMATRA ili waweze kuona nini cha kufanya
ili walau kuliweka sawa la staend hiyo.
PICHA NA HABARI NI KWA HISANI YA JOHN BANDA, DODOMA
0 comments:
Post a Comment