Home » » Msikiti wa Answar Sunna wa Mjini Dodoma uliteketea kwa Moto jana.

Msikiti wa Answar Sunna wa Mjini Dodoma uliteketea kwa Moto jana.


Msikiti mkubwa wa Answar Sunna uliopo barabara ya saba mjini Dodoma umewaka moto mchana huu ikiwa ni muda mfupi baada ya swala ya mchana kumalizika....

Akiongea kwa njia ya simu na Mpekuzi wetu, mmoja wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la msikiti huo...

Hata hivyo, shuhuda mwingine aliyeongea na mtandao huu amedai kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia ghorofa ya juu ya jengo hilo. 
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, moto huo umefanikiwa kudhibitiwa na jeshi la zima moto na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha kutokana na moto huo.
PICHA NA VIJIMAMBO BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa