SERIKALI na taasisi zisizo za kiserikali zimetakiwa kulisaidia kundi la
wajane na watoto yatima ambalo kwa muda mrefu limekuwa likisahaulika katika
jamii.
Wito huo ulitolewa mjini hapa jana na Mchungaji wa Jumuiya ya Kikristo
Tanzania (CCT), Dk. William Kopwe alipokuwa akifungua semina ya wajane kitaifa
iliyofanyika Chuo Kikuu cha St. John.
Dk. Kopwe alisema wajane na yatima wamesahaulika katika kupatiwa huduma
mbalimbali hali inayowafanya kujiona wanyonge na kukata tamaa.
“Kundi hili limesahaulika hata kanisani, wakati hayo ni maagizo ya Mungu
kusaidia wajane na yatima…yeye anayeonea wajane na yatima na alaaniwe, haya ni
maneno kutoka katika maandiko matakatifu,” alisema.
Alisema umefika wakati kwa Watanzania kumgeukia Mungu na kutimiza
maagizo yake kwa kuwasaidia watu hao, ili waweze kushiriki katika fursa
mbalimbali.
Mwenyekiti wa huduma inayoshughulika na wajane, yatima na wanafunzi,
Witness Msuya, alisema lengo la huduma hiyo ni kuwajenga wanafunzi kiroho,
kuwatia moyo na kuwafundisha jinsi ya kutafuta miradi mbalimbali ya ujasiriamali.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment