Kinamama hawa wanasubiri muda wao wa kujifungua, lakini wanaongezewa uchungu kwa kuishi na wadudu wasumbufu, wanaonyonya damu zao.
Kama ilivyo kwa kiwanda au mashine inavyotumika
kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali, ndivyo ilivyo kwa mwanamke,
kiwanda mahsusi cha kutengeneza binadamu mpya, yaani mtoto.
Ni ukweli usiopingika kuwa licha ya mchango mkubwa
ambao hupatikana pia kwa mwanamume katika uumbaji wa mwanadamu, lakini
bado mchango wa mwanamke ni mkubwa zaidi ya ule wa mwanamume.
Maumbile asili ya mwanamke ndiyo humfanya aendelee
kuwa kiwanda cha kumfinyanga mwanadamu mpya na kumleta duniani kwa
uwezo wa Mungu na utaratibu wake.
Ili yote yafanyike kwa umakini na umaridadi,
mwanamke mjamzito anahitaji mazingira mazuri yenye kumpa faraja na
matumaini na hata kumwondolea mawazo ya jinsi gani itakavyokuwa siku ya
mwisho ya siku zake 270 au miezi tisa kama ilivyozoeleka za kubeba
mimba.
Maandalizi hayo kwa mjamzito yanakwenda sambamba
na tumaini la furaha yake pamoja na nderemo kwa jamii inayomzunguka
ambayo kila mmoja wake wakati wote huwa na mategemeo ya kupata kiumbe
kipya.
Ni kutokana na hilo, bado kuna msisitizo kuhusu maandalizi ya kina kutoka kwa familia au jamii anayotoka mwanamama huyo.
Serikali kwa upande wake pia inalo jukumu la
msingi la kujiandaa na kumsaidia mama huyo katika kumwekea mazingira
mazuri na salama wakati wa kujifungua.
Mjini Dodoma, kipo kituo maalumu kilichojengwa kwa
ajili ya kuwapa afueni wanawake wajawazito hasa wale ambao muda wao wa
kujifungua umekaribia ili wawe karibu na huduma zote muhimu ikiwamo
hospitali.
Kituo hicho ambacho kipo Kata ya Majengo katikati
ya mji, kimepewa jina maalumu, Chigolela, jina ambalo kwa Kigogo, watu
asili wa mji na mkoa huo, lina maana ya mimba iliyopitiliza muda wake wa
kujifungua.
Chigolela ya Dodoma ambayo ilijengwa kwa ajili ya
kutoa huduma kama nilivyoeleza hapo juu, imegeuka na kuwa sehemu ya
gereza la tabu na mateso kwa wanawake, kiasi cha kukimbiwa na wanawake
wengi ambao huamua kukaa majumbani au kupanga katika nyumba kwa ndugu
zao wengine.
Majira ya asubuhi naingia katika kituo hicho kwa
ajili ya kushuhudia kile nilichokuwa nikiambiwa kama kina ukweli kiasi
gani ndipo ninakutana na hali ambayo kimsingi haielezeki.
Chanzo;Mwananchi.
Chanzo;Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment