Home »
» CRDB KUANZISHA MRADI WA NYUMBA
CRDB KUANZISHA MRADI WA NYUMBA
Benki ya CRDB tawi la
dodoma mjini kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya bahi mkoani
hapa inatarajia kuanzisha mradi wa kuwajengea nyumba za gharama nafuu
wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo yalibainishwa juzi na meneja
wa benki hiyo, rehema hamisi wakati akizungumza katika kikao cha baraza
la madiwani katika wilaya hiyo na kuongeza kuwa mradi huo utawawezesha
wakazi wa halmashauri hiyo kuondokana na nyumba za tembe na kujengewa
nyumba za kisasa kwa gharama ya kati ya shilingi milioni 5 hadi 6 ambapo
watatakiwa kurejesha kwa muda wa mwaka mmoja hadi miaka mitano.
Alieleza
kuwa baadhi ya wananchi wenye kipato cha chini hawawezi kuweka pesa
kiasi cha kutosha kujengea nyumba kwani pesa zao huishia kununulia
chakula tu hivyo waliona ni vyema kushirikiana nao katika ujenzi wa
nyumba hizo ili kuwawezesha kupata makazi bora na yenye hadhi.
"Hapa
tumewalenga wananchi wenye kipato cha chini kabisa yaani wakulima na
wafugaji ambao kutokana na kipato chao hawawezi kujenga nyumba za kisasa
lakini wana uwezo wa kupata pesa pindi wanapouza mazao yao," alisema
hamisi.
Aidha aliwataka madiwani hao kuwaelimisha wananchi wao
taratibu za kupata mradi huo ili waweze kujengewa nyumba hizo ikiwa ni
pamoja na kuunda vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali pamoja na vyama
vya kuweka na kukopa (saccos).
Naye mkuu wa wilaya ya bahi, betty
mkwasa, alisema lengo la kuialika benki hiyo kuanzisha mradi huo
wilayani hapo ni kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini kujenga
nyumba nzuri za kisasa za kuishi kwani wengi wao hawana uwezo wa kujenga
nyumba lakini wakikopeshwa wanaweza kulipia mkopo huo
CHANZO MAJIRA
0 comments:
Post a Comment