Wabunge
Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless
Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake
ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing)
kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii.
Lema
akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo
yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu
hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao
unapaswa kuhojiwa.
Gazeti
hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto
akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge
wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye.
Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akisema:
“Mimi sikumtaja mtu, kwahiyo kama kuna mtu analalamika hilo ni suala jingine, ila mimi nilimaanisha nilichokisema”.
Hata
hivyo, Zitto alieleza kuwa msimamo wa Lema ulikuwa unapingana na
wabunge wengine wa Chadema, ambao waliwahi kupendekeza kuwa posho
zifutwe.
Zitto
alisema kuwa yeye mwenyewe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.
“Mimi
sipokei posho kabisa, posho za vikao na ndiye mbunge pekee ambaye
hapokei posho ya vikao tangu mwaka 2011,” aliongeza Zitto, ambaye
anahudhuria mkutano unaozungumzia uendeshaji wa Serikali kwa uwazi huko
London, Uingereza.
Zitto
alisema malipo ya wabunge mpaka sasa ni makubwa sana ukilinganisha na
hali ya wananchi wakati Serikali ikishindwa kulipa vizuri walimu na
wauguzi.
“Hatuwezi
sisi kama wabunge kuanza kulilia posho, wakati wananchi wetu hawana
maji, hatuwezi kulilia posho. Mbunge anayetaka posho zaidi akafanye kazi
nyingine na awaachie wanaoweza kuwakilisha watu waendelee,” alisema
Zitto.
Lema,
hata hivyo, alisema kwamba katika mkutano huo aliweka bayana kwamba
umasikini siyo uzalendo na kusisitiza kuwa wabunge wanapaswa kuwa na
maslahi bora na wakati huohuo wana wajibu wa kuwatetea watumishi wengine
wa umma.
“Nilisema
huwezi kuzuia taasisi moja kupewa maslahi bora eti tu kwa sababu
watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni haki wabunge kulipwa vizuri na
wakati huo wapiganie maslahi ya watumishi wengine,” alisema Lema na
kuongeza:
CHANZO;MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment