Dodoma. Mkutano wa 13 Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania uliomalizika juzi mjini Dodoma, umeandika historia
mpya kutokana kuwapo kwa mambo makuu manne yaliyolipa Bunge hilo sura
tofauti na mikutano mingi iliyopita.
Mambo hayo ni pamoja na tukio la nadra la muswada
wa Serikali kuungwa mkono na pande zote ndani ya Bunge, kukataliwa kwa
mapendekezo ya marekebisho kandamizi katika Sheria ya Magazeti ya 1976,
kuwapo kwa mjadala mpana kuhusu mambo ya dharura na hotuba ya Rais
Jakaya Kikwete iliyotoa msimamo kuhusu uanachama wa
Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Hata hivyo, kuna mambo kadhaa ambayo yamebaki
viporo yakisubiri kuingizwa katika ratiba ya mkutano wa 14 uliopangwa
kuanza Desemba 13 mwaka huu, ukihamishwa kutoka Februari 2014 ili
kupisha Bunge Maalumu la Katiba ambalo litaketi kati ya Januari na
Machi, mjini Dodoma.
Mambo hayo ni kujadiliwa kwa Sheria ya Kura ya
Maoni ambayo ilifanyiwa marekebisho makubwa, mrejesho wa Kamati Teule ya
kuchunguza migogoro baina ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa
ardhi.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment