Dodoma. Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na
Maliasili inayoongozwa na James Lembeli, inatarajiwa kuwasilisha taarifa
yake Ijumaa siku ambayo Mkutano wa 14 wa Bunge utamaliza shughuli zake.
Taarifa zilizopatikana bungeni jana, zilisema kuna
uwezekano kamati hiyo ikatumia nafasi hiyo kuwasilisha taarifa ya
kamati yake ndogo iliyochunguza mwenendo wa Operesheni Tokomeza
Ujangili.
Hata hivyo, kumekuwa na wasiwasi kuwa ripoti hiyo
inaweza kutowasilishwa bungeni hasa kutokana na mambo mazito
yanayotarajiwa kuibuliwa yanayoweza kusababisha baadhi ya mawaziri
kung’olewa.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana, zilieleza
kuwa wajumbe wa kamati hiyo ndogo ya uchunguzi ya Kamati ya Bunge la
Ardhi, Mazingira na Maliasili imejichimbia Hoteli ya St. Gasper
ikikamilisha ripoti yake. Kamati hiyo imezua hofu kubwa ndani ya Wizara
ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo zinazotarajiwa
kuguswa na ripoti hiyo.
Ni ripoti kama hii inayotarajiwa kuwasilishwa
bungeni Ijumaa ndiyo iliyomng’oa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii, Ezekiel Maige kutokana na kashfa ya ugawaji vitalu vya uwindaji.
Tayari, Kamati ya Lembeli iliyoanza kazi Novemba 25 imekamilisha kazi
ya kuhoji watu mbalimbali, wakiwamo mawaziri watatu ambao wizara zao
zilihusika moja kwa moja na operesheni hiyo.
Mawaziri waliohojiwa katika Hoteli ya Bahari Beach
Dar Es Salaam ni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis
Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alipoulizwa jana alisema hana uhakika ila upo uwezekano wa ripoti hiyo ikawasilishwa Ijumaa.
sambamba na taarifa ya kamati mama ingawa hakuwa
na uhakika. Miongoni mwa wanadaiwa huenda ripoti hiyo ikawang’oa ni Dk
Mathayo na naibu wake.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment