MEYA wa Manispaa ya Dodoma, Emanuel Mwiriko, amewataka madiwani kutoa taarifa sahihi za kimaendeleo katika kata zao.
Mwiriko alitoa agizo hilo juzi alipokuwa akipokea taarifa mbalimbali
za maendeleo zilizowasilishwa na madiwani wa manispaa hiyo.
Aliwataka madiwani kuwa na agenda muhimu ya kujadili kwa kima mambo ya kimaendeleo badala ya kuwa na propaganda.
Wakati huohuo madiwani walisema mji wa Dodoma unashindwa kuendelea kwa
kasi kutokana na manispaa kukosa ardhi, kwani iliyopo inamilikiwa na
Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA).
Madiwani hao walisema licha ya CDA kuwa na wajibu wa kuboresha mji wa Dodoma, imekuwa kinyume.
Diwani wa Kikombo, Emmanuel Maanyonyo (CCM), akiwasilisha taarifa ya
maendeleo alisema kata hiyo ina shule tano ambazo zinakabiliwa na
upungufu wa matundu ya vyoo pamoja na uhaba wa walimu.
Alisema kutokana na hali hiyo wanafunzi wanakosa fursa ya kupata eimu
bora ikiwa ni pamoja na kukosa vipindi muhimu kutokana na kukosekana kwa
walimu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo, alisema wananchi
katika kata mbalimbali wanaoonekana kupinga masuala ya kimaendeleo
wapigwe.
Kauli hiyo ilizua utata na madiwani kumtaka mkurugenzi huyo kutoa
ufafanuzi kama sheria ya nchi inaruhusu kuwa mtu akifanya kosa anatakiwa
kupigwa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment