Spika wa Bunge,Anne Makinda
Malalamiko ya wabunge yalitolewa kwa nyakati tofauti bungeni baada ya kuwasilishwa kwa taarifa tatu za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema Jumamosi kuwa mawaziri husika watatakiwa kujibu hoja mbalimbali za wabunge hapo kesho.
Kuwasilishwa kwa taarifa hizo kulikoibua vitendo vingi vya ufisadi, ubadhirifu na upendeleo wa kuhamishia wabadhirifu maeneo mengine ya kazi, kuliwafanya wabunge kuchachamaa na kutamka kwamba Waziri Mkuu Pinda atimuliwe kazi kwa kushindwa kuzuia upotevu mkubwa wa fedha za umma unaofanywa serikalini.
Walimtaka pia Waziri Ghasia kutimuliwa kwa maelezo kuwa wizara yake imekithiri vitendo vya ufisadi katika halmashauri mbalimbali nchini.
Mwenyekiti wa Kamati za Hesabu za Serikali za Mitaa, Rajab Mohammed Mbarouk, alisema wakati akiwasilisha taarifa yake kuwa kuna ushirikiano wa hali ya juu kutekeleza dhamira ovu kati ya Hazina, Tamisemi na halmashauri husika kwa kuwapo kwa mtandao wa kutisha wa kifisadi baina ya mamlaka hizo za Serikali.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge, katika taarifa yake kuhusu utekelezaji wa majukumu ya kamati katika kipindi cha Februari hadi Desemba mwaka huu, alisema kwa ujumla lengo la makusanyo ya fedha kutoka vyanzo mbalimbali halikufikiwa kwa kiasi cha asilimia 14.3.
Alisema kamati yake ilijulishwa katika robo hiyo ya kwanza ya mwaka 2013/14 jumla ya mapato yote yalifikia Sh. bilioni 3,082.2 sawa na asilimia 85.7 ya makadirio ya Sh. bilioni 3,598.5.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma, Kabwe Zitto, aliibua dosari kadhaa zilizotokeza katika ukaguzi wao kwa kutozingatiwa kwa utaratibu wa kuanzishwa vitengo vya manunuzi na utayarishaji usiokuwa sahihi wa mipango ya mwaka ya manunuzi.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment