Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akisisitiza jambo alipo kuwa
akiongea na Uongozi wa ngazi mbali mbali za Mkoa na baadhi ya vijana wa
mkoa wa Dodoma waliokabidhiwa heka 50 za mashamba ya ushirika.
Mkuu
wa Mkuu wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi Bibi Rechal Chuwa, Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa na
Mkuu wa Magereza Wilaya ya Bahi Bw; Ramadhani H. Mabere wakiwa
wameshika zana zao za kazi tayari kusaidiana na vijana zaidi ya 100
kusafisha shamba lenye heka 50 la vijana hao.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akimsikiliza kwa Makini alie kuwa
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Bahi Bw Sustenance Mpandu alipo amua
kuachana rasmi na Chama chake na kuungana na vijana wapenda maendeleo wa
Mkoa wa Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi alie vaa sare ya timu ya Taifa
katikati na kulia kwakwe ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty C. Mkwasa
wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mbali mbali pamoja na
baadhi ya vijana wapenda maendeleo wa Mkoa wa Dodoma wakiinua zana zao
za kilimo juu kuashiria kuwa Uhuru ni Kazi. Habari & picha na Madau
Sixmund J. Begashe
Vijana
nchini wametakiwa kuacha tabia ya kutumika na kutumia nguvu na akili
zao kwa manufaa ya wachache bali wazitumie kwa manufaa yao na ya Taifa
kwa ujumla kama ishara sahihi ya ukombozi wa vijana kifikra na kutambua
kuwa Uhuru ni Kazi.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi katika
maadhimisho ya aina yake ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania kimkoa yaliyo
fanyika wilayani Bahi, Dr Nchimbi aliwapongeza vijana hao zaidi ya mia
moja walio jikomboa kifikra kutoka vyuo vikuu, wahitimu na waendesha
Boda Boda wa Mkoani hapa kwa kufanya maamuzi ya busara na kuondokana na
fikra potofu za ajira bora ni ile ya kuajiriwa.
Dr
Nchimbi alisisitiza kuwa vijana sasa waachane na Maandamano yenye sura
ya uvunjifu wa amani bali maandamano hayo yawe ni yakuelekeza nguvu zao
katika kujiajiri wenyewe kama walivyo fanya vijana wa Mkoa wa Dodoma kwa
kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wao kwa kujiweka huru kifikra na
kujitafutia fursa za kimaendeleo.
Kama
kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inavyo sema Vijana ni Nguvu ya
Saraslimali watu Tuwaamini na Tuitumie kwa Manufaa ya Taifa letu, Dr
Rehema Nchimbi ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma
kushirikiana na vijana wote watakao kuwa huru kifikra na kujitambua kuwa
wao ni raslimali muhimu ya Taifa letu.
Katika
sherehe hizo zilizo pambwa na Mapanga, Nyengo na vifaa mbali mbali vya
kilimo, mmoja wa kati ya viongozi wa Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
wilaya ya Bahi ambae ni mwanachuo katika chuo kikuu kimoja wapo Bw
Sustenance Mpandu, aliungana na vijana wenzake baada ya kukiri kwamba
amekuwa huru kifikra na hivyo kuachana na utamaduni wa kupotosha kila
kweli, Utamaduni ambao ulimfubaza kifira na hivyo kushindwa kuona fursa
nyingi ambazo vijana wanaweza kuzitumia kwa maendeleo yao na Taifa kwa
ujumla.
Bw
Mpandu alisema kuwa yeye ni mmoja wa watu walio kuwa mstari wa mbele
katika kupinga ukweli na kujitahidi kuufanya uongo uwe ukweli masikioni
mwa watanzania, lakini sasa ameona alicho kuwa akikifanya ni dhambi
kubwa na hakina tija kwa maslai ya Taifa hili.
Alie
kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA alitoa wito kwa vijana wote na wasomi
wote nchini kuachana na dhambi ya kupotosha Ukweli kwa ajili ya maslahi
ya wachache bali waungane na Serikali katika kuwaletea wanachi maendeleo
na si kuikosoa serikali kila kukicha huku wakijua ukweli kuwa serikali
imejitahidi sana kuwaletea wananchi wao maendeleo ndani ya miaka hii 52
ya Uhuru wetu.
Mkuu
wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa licha ya kuwapongeza vijana hao kwa
kujikomboa kifikra aliwaahidi kuendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha
wanafikia malengo yao, pia aliwashauri kufanya kazi kwa bidii ili
mafanikio watakayo yapata kutoka kwenye mashamba hayo yaweze kutoa fursa
kwa vijana wengine hususani ya kuwaajiri.
Kwa
niaba ya Vijana hao walio jikomboa kifikra Bw.Anyelwisye Jonas
Aliupongeza uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa kuungana nao bega kwa bega
katika safari yao hiyo ya ukombozi wa kifikra na kuhaidi kuwa watakuwa
mabalozi kwa vijana wengine wenye mitazamo finyu ya kusubiri ajira ya
Serikali na penginepo badala ya kujiajiri na wao kuwa waajiri wa
wengine.
Katika
maadhimisho hayo, Viongozi mbali mbali wa Mkoa na Wilaya walijitole
pasa za kusafisha heka zote 50 na Mkururugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
kupitia Mkurugenzi wake Bi Rechal Chuwa kuahidi kuwajengea mahali
atakaae kaa mtu atakae ajiriwa na vijana hao kwa ajili ya uangalizi wa
shamba litakalo kuwa na mazao na mifugo.
Chanzo;Michuzi blog




0 comments:
Post a Comment