Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoa
Dodoma, wameulalamikia uongozi wa serikali yao kujenga makaburi feki pasipo
kuwashirikisha wahusika wa makaburi hayo.
Wakizungumza wananchi hao wamemtupia lawama mtendaji wa kijiji YONA
MGANGA, na kusema kuwa serikali imeamua kuhamisha makaburi bila
kufuata utaratibu.
Akizungumza EMANUELL MKIGA mmoja
wa vijana walio pata tenda ya uhamishaji wa makaburi hayo ameelezea jinsi zoezi
hilo la ujenzi wa makaburi feki lilivyofanyika katika kijiji hicho kwa kusema
kuwa walilipwa shilingi elfu tisa kwa ajili ya ujenzi.
ARFEDI NDEGEULAYA Mwenyekiti wa kijiji cha mpwapwa
amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa yeye anafanya jitihada
mbalimbali ili kumaliza tatizo hilo katika kijiji chake.
Chanzo;jiachie blog
Chanzo;jiachie blog
0 comments:
Post a Comment