Home » » Mwanazuoni akerwa na wanasiasa

Mwanazuoni akerwa na wanasiasa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

.Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Benadetha Kilian amekerwa na tabia ya wanasiasa ya kuteka mjadala wa katiba akisema kitendo hicho kitazaa Katiba mbovu.
Profesa Kilian alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa akichangia hotuba ya Seneta Amos Wako alipolihutubia Bunge hilo kuhusu historia ya namna nchi ya Kenya ilivyoweza kutengeneza katiba yao.
Kiliani alionyesha mashaka makubwa akisema kuwa hadi sasa dalili zinaonyesha kuwa mchakato wa katiba unabebwa kwa seheumu kubwa na wanasiasa jambo linaloonyesha kufunikwa kwa mawazo ya wengine.
Msomi huyo alimtaka Wako kutoa maelezo ya kina kwa wajumbe ni namna gani nchi ya Kenya ilivyofanikiwa kupunguza nguvu ya wanasiasa na kuruhusu mawazo ya makundi mengine.
“Kuna tabia ya wanasiasa na vyama vya siasa kuteka nyara mawazo na michakato ya watu wengine, ningependa kujua kwa uzoefu wako katika nchi yetu mlitumia njia zipi katika kupunguza makali ya watu hao,”alisema Kiliani.
Alitahadharisha wajumbe wenzake kuwa makini na masuala ya wanasiasa katika mchakato mzima wa utungwaji wa katiba kwa kuwa inaweza kusababisha kuficha kabisa mawazo ya wananchi.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hiyo, Seneta Wako alisema kuwa katika maeneo mengi suala la wanasiasa katika utungwaji wa katiba haliepukiki.
Wako alisema kitu cha msingi kinachowezaa kuangalia ni jinsi gani mawazo ya wananchi yameingizwa na kupewa nafasi yake kuliko kulundika mawazo na mitazamo ya wanasiasa.
Aliwataka wajumbe wa bunge hilo kuangalia jinsi ya kuingiza mawazo ya wanasiasa lakini yakiwa nyuma ya mawazo ya wananchi ambao ndio wenye katiba.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa