SERIKALI imetoa
ufafanuzi juu ya vitambulisho vya waandishi wa habari ( Press card) wakati wa
Bunge Maalum la katiba na kusema kuwa ndicho kigezo pekee kitakachowezesha waandishi wa habari kutimiza majukumu yao
vyema katika kipindi chote cha bunge
hilo.
Hayo yamesemwa
leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene wakati akitoa tamko la Serikali
kufuatia taarifa potofu zilizoripotiwa
na baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini.
Mwambene
alibainisha kuwa utaratibu wa kutoa
vitambulisho hivyo si mgeni kama
ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba unaweza kukipata ndani ya
saa 24 ikiwa tu mwandishi anakidhi vigezo. Alisema vitambulisho
vinatolewa tu kwa mwandishi mwenye taaluma ya uandishi wa habari kutoka chuo
kinachotambulika naSerikali kwa kuzingatia sheria na kanuani zilizowekwa.
Alisisitiza kuwa utaratibu wa kutoa vitambulisho kwa waandishi habari upo na ni wa kisheria hivyo ni lazima ufuatwe. Pia alisema kuwa ni vyema kila mwandishi akafuata
taratibu zote za kupata kitambulisho kinachotolewa na MAELEZO kwa kuwa bila
kitambulisho hicho hataweza kufanya kazi
katika kazi rasmi kama vile Bunge maalum la katiba.
Alitoa wito kwa waandishi wa habari kujiendeleza
katika taaluma ya uandishi wa habari kwa wale wasio na sifa za kupewa
vitambulisho hivyo ili kuiniua Sekta ya Habari hapa nchini

0 comments:
Post a Comment