Home » » MAZUNGUMZO YAEPUSHA MGOGORO UDOM

MAZUNGUMZO YAEPUSHA MGOGORO UDOM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Viongozi wa Shule za Sanaa, Lugha na Sayansi za Jamii ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wameanza mazungumzo na viongozi wa Serikali ya wanachuo wa shule hizo, kupata suluhu ya utata uliyojitokeza katika kuwapatia mikopo yao ya tafiti na mafunzo kwa vitendo.
Taarifa hizo zilitolewa kwa NIPASHE jana na Rais wa Wanachuo hao, Masatu Kyabwene, na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa wanaosomea Shahadaya kwanza, Profesa Peter Msoffe.

Kyabwene alisema viongozi wa wanafunzi katika mazungumzo ya jana,walitumia barua zao za kuomba sehemu za kujifunzia kwa vitendo, walizopewa na chuo kama uthibitisho kwamba inafahamika kuwa wanasitahili kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo.

Alisema mgomo uliyokusudiwa kufanyika jana umesitishwa kusubiri hatma ya mazungumzo hayo.
Awali, Kyabwene alieleza mpango wa wanachuo hao kufanya mgomo na maandamano jana kwa lengo la kupaza sauti, dhidi ya alichokiita manyanyaso.

Sababu zilitajwa kuwa ni kudai mikopo ya wanaosomea Sayansi za Jamii,waliyopelekewa na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)lakini uongozi ukadai hawasitahili, fedha zitarejeshwa zilikotoka.“Hata wanaosomea Sanaa za Lugha ambao tulielezwa kwa ufupi tu kwamba fedha zao hazikuletwa, tunahitaji kufahamishwa kwa ufasaha nini kinaendelea na hatma yao itakuwaje,” alieleza Kyabwene
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa