Home » » CHEYO: SISI NI NDUGU, WATOTO WA BABA MMOJA

CHEYO: SISI NI NDUGU, WATOTO WA BABA MMOJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Ndugu wa kuzaliwa ambao ni wajumbe wa Bunge la Katiba, John na Isaack Cheyo, juzi waliongozana kutoa tamko linalozungumzia Mkutano wa Rais Jakaya Kikwete na uongozi wa vyama vya siasa.
John Cheyo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP) na Isaack ni mdogo wake na mwanachama katika chama hicho ambaye naye aliteuliwa na Rais kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba.
Juzi, Cheyo mkubwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), alikutana na waandishi wa habari kuwajulisha kuwa Rais Kikwete amekubali ombi la vyama vya siasa la kukutana naye ili kujadili kuhusu mchakato wa Katiba.
Cheyo alisindikizwa na mdogo wake pamoja na Fahm Dovutwa wa UPDP, lakini msemaji alikuwa ni Cheyo mkubwa.
Kumekuwapo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu ambao huwatuhumu wanasiasa kuwa wanabebana katika kupeana nafasi za uongozi ndani ya vyama na hata katika nafasi za uwakilishi.
 Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa