Home » » VITAMBI VYOTE UWANJA WA JAMHURI

VITAMBI VYOTE UWANJA WA JAMHURI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Kila alfajiri ukifika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, huwezi kuwakosa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba uwanjani hapo.
Kuwapo kwao pamoja na watu wengine si kwa ajili ya mkutano wala nini. Hufika ‘kupunguza vitambi’ kwa kufanya mazoezi ya viungo.
Hapa wengine hutembea kuzunguka uwanja wa mpira mara kadhaa, wengine hukimbia na wengine hujiunga na kundi la mazoezi ya viungo ambalo hutumia uwanja wa mpira wa mikono kwa ajili hiyo.
Miongoni mwa wasiokosekana uwanjani hapo ni Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja ambaye pia ni mchezaji katika timu ya soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo, wakati huu wa Bunge Maalumu, wadau wa mazoezi siyo wengi kama inavyokuwa wakati wa Bunge la Jamhuri. Labda ni kwa sababu Bunge hilo halina timu za michezo zaidi ya wajumbe kusuguana ndani ya kamati.
 Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa