Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKATI Tatizo la Ombamba nchini limekuwa sugu huku jitihada za
kulitatua bado hazijafanikiwa, Ombaomba mkoani Dodoma wamekiri kuwa
Ijumaa yoyote kwao wameifanya kuwa siku ya mshahara hivyo watendaji
wasiwabughudhi.
Wakizungumza wakiwa kwenye msururu wa kugawiwa ‘Uji na Unga kibaba
kimoja mkoani hapa jana, pembeni kidogo mwa Msikiti wa Nunge karibu na
Hoteli ya Wimpy, Ombaomba hao walidai, wanataka wasibughudhiwe kwa
sababu siku hiyo ni siku ya malipo na mshahara kwao.
Walipoulizwa ni nani anayewalipa mshahara wakati hawafanyi kazi ila
kuomba, walijigamba wakisema kama wafanyakazi wengine wanavyolipwa na
waajiri wao, nao wana Waajiri wao barabarani ambapo watu wenye mapenzi
mema na roho nzuri, huwapatia chochote walichonacho.
“Kama ninyi mnavyodai na kuandamana mnapocheleweshewa mishahara, hata
sisi siku ya Ijumaa ambapo Wa-Islamu na watu wenye mapenzi mema,
hutupatia zaka zao ikiwa ni pamoja na Chakula, Fedha na Nguo.
Tunashangaa Askari na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji wa Dodoma
wanapotuondoa barabarani wakati tupo kwenye meli moja ya kujitafutia
riziki! Tofauti yetu ni kwamba, wao wanaomba kwa kufanya kazi, sisi
tunaomba kwa kusaidiwa”.alisema Mama aliyejita Mdala Roda.
Utafiti uliofanywa 2013 na Shirika linashughulika na masuala ya
Familia na Afya (FHI360) chini ya mradi wa Pamoja Tuwalee; Kati ya
watoto 332 waliohojiwa, asilimia 35.5 sawa na watoto 118, walibainika
wanatoka Dodoma;
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment