Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Aidha, maofisa hao wametakiwa hadi kufikia Machi 31, mwaka huu wawe
wametoa taarifa wizarani kuhusu wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao
shule ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Agizo hilo lilitolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alipokuwa akizungumza katika siku
ya kupinga ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wanawake, iliyofanyika
mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
“Ofisa maendeleo ya jamii yeyote ambaye vitendo hivi vitatokea
katika eneo lake tutamchukulia hatua, lazima waongeze jitihada hata kama
kuna changamoto ya rasilimali fedha na vitendea kazi,” alisema.
Mwalimu alisema maofisa hao wanatakiwa kuwatumia watendaji wa
kata na vijiji kupata taarifa na kuhakikisha hatua sahihi zinachukuliwa
ili kukomesha ukeketaji.
Alisema katika malengo yake, Tanzania imejiwekea itakapofika mwaka 2030 kusiwe na mtoto yeyote ambaye atakeketwa.
“Serikali haitakubali kutumia kigezo cha mila na desturi kuendeleza
vitendo vya ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wanawake kwani vina
madhara makubwa kiafya, kielimu, kisaikolojia na kimaendeleo,” alisema
waziri huyo.
Alisema ukeketaji ni janga la kitaifa, hivyo ni lazima mapambano
yake yawapo ili kutokomeza vitendo hivyo, kwani wa utafiti wa
kidemografia na afya Tanzania uliofanyika mwaka 2010 katika mikoa mitano
umeonyesha ukeketaji upo kiwango cha juu.
Aliitaja mikoa inayoongoza kwa vitendo hivyo kuwa ni Manyara
asilimia 71, Dodoma asilimia 64, Arusha asilimia 59, Singida asilimia 51
na Mara asilimia 40, na kote vimetokana na imani na mila potofu.
Alisema mila hizo zimeanza kujitokeza katika mikoa mingine kama
Dar es Salaam, Morogoro na Pwani, kutokana na watu wa makabila
mbalimbali kuhamia mikoa hiyo.
Aliwataka maafisa hao kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha
wanamkamata mzazi au mlezi au mtu yeyote anayefanya vitendo vya
ukeketaji na kesi hizo zitasimamiwa ipasavyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) kwa
kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA),
Cynthia Mushi, alisema bado kuna changamoto katika kukabiliana na
vitendo hivyo kutokana na kukosekana miundo na mifumo ya ulinzi.
Alisema hali hiyo inaweza kutoa ulinzi wa kutosha kwa wasichana
walio katika hatari na walioathirika na ukeketaji na mila kandamizi.
CHANZO:GAZETI LA
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment