Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo imekutana na
kuendelea na kuujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kwa
kuendelea kupitia kifungu kwa kifungu katika Muswada huo.
Akifungua
kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Peter Serukamba alisema
wamekuta katika kikao hicho ikiwa ni muendelezo wa kupitia Muswada huo
kwa makini kabla ya kupelekwa Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na
wabunge.
Aliongeza
kuwa ni wakati kwa wajumbe kuendela kuujadili kutoa maoni yao katika
kuuboresha Muswaada huo ili waweze kupeleka Muswada ambao utaleta Sheria
iliyobora kwa mufaa ya tasnia ya habari na watanzania kwa ujumla.
“Wajumbe
nawaomba tuujadili na kuuchambua Muswada huu kwa makini sana kwani sisi
ndio watungaji wa sheria na tutuo maoni na marekebisho yatakaoufanya
Muswada huu kuwtoa Sheria iliyo bora” alisisitiza Mhe. Serukamba.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau habari kupitia barua pepe ya cna@bunge.go.tz.
0 comments:
Post a Comment