Na Daudi Manongi,MAELEZO.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Haji Semboja amewataka wamiliki na
wadau wa tasnia ya habari hapa nchini kuusoma na kuelewa madhumuni ya Muswada
wa Huduma za Habari kwa ajili kusaidia maoni ambayo yataboresha muswada huo.
Profesa
Semboja asema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa
habari hizi.
Amesema
ni vema wanahabari na wadau wa habari wakausoma kwa kina na kutoa maoni yao kwani
hakuna sababu ya kuuchelewesha muswada huo kwa ajili ya kuimarisha tasnia ya
habari.
Profesa
Semboja ameipongeza Serikali kwa kuwa na uwazi katika kuuleta muswada huu kwa
jamii ili wauone na kuulewa na waweze kutoa maoni yao ili tupate kitu kilicho
bora.
Amesema
kuwa baadhi ya maeneo yaliyomo katika muswada huo yatasaidia wanahabari kuboresha
taaluma yao na kuwa na wanahabari wanaotambulika.
Profesa
Semboja amewataka wana habari kuusoma vyema muswada huo na kuacha kuwa na
mawazo hasi huku akisisitiza ushiriki wao uwe mkubwa kwani muswada huu
unapatikana kwenye mitandao na hivyo unamfikia mtu yeyote kwa urahisi kabisa.
Muswada
wa Vyombo vya Habari ulichapishwa na kuwekwa hadharani tangu Septemba 2016,
pamoja na mambo mengi mazuri wadau wakuu wote walishiriki katika hatua za ndani
za serikali kutoa maoni na kwa sasa wanashiriki katika hatua ya Kamati ya Bunge.
0 comments:
Post a Comment