NAIBU Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha, amewataka
viongozi wa vyama vya ushirika kuhakikisha mali za vyama hivyo
zinawanufaisha wanachama na kukuza uchumi wa chama.
Alisema uchumi ukikua utaviwezesha vyama hivyo kujitegemea,
kujiendesha kibiashara na kurejesha umiliki kwa wanachama kulingana na
maadili na misingi ya ushirika.
Aidha, aliiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika iweke mfumo maalumu wa
kumbukumbu wa kufuatilia mali za vyama vya ushirika kuzilinda na
kuhamasisha wananchi wa rika mbalimbali kujiunga.
Ole Nasha alitoa agizo hilo wakati akifungua kikao cha kazi cha siku
tatu cha wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu, miradi ya pamoja na wa
benki za ushirika nchini, kilichoanza jana mjini hapa.
Aliwataka viongozi hao kuhakikisha mali za wanaushirika zinalindwa kisheria kama vile kuwa na hati.
Aliwakemea wanaouza mali hizo kiholela kwa wenye mali na kutaka
ushirika uendeshwe kwa uwazi na ufanisi. Alitaka wawapunguzie wanachama
michango kwa ajili ya kuendesha shughuli za chama kuanzia ngazi ya
msingi hadi shirikisho na kuwa na vyanzo vya mapato vya ndani, ili
kuondoa utegemezi wa mikopo.
“Ni muhimu kutambua na kuanzisha mpango mkakati wa kuongezea thamani
mazao ya wanachama kama vile kuanzisha viwanda vidogo na vya kati. Hii
itawaongezea kipato, ajira, kupunguza upotevu wa mazao na pia itakuwa ni
mchango wenu katika kutekeleza azma ya serikali ya ujenzi wa uchumi wa
viwanda,” alisema Ole Nasha.
Aidha, aliiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika iweke mfumo maalumu wa
kumbukumbu wa kufuatilia mali za vyama vya ushirika ili kuzilinda dhidi
ya ubadhirifu na upotevu, kuweka na kuimarisha huduma ndani ya vyama
vya ushirika ili kuvutia wananchi wa rika mbalimbali kujiunga.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment