Na Evelyn Mkokoi – Mwandoya Meatu
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye Pia ni Mbunge wa
jimbo la Kisesa Wilayani Meatu, amesema waowabeza Mawaziri wa Rais Magufuli na
kusema kuwa wanamuogopa na kuwa hawawezi kumshauri wamechemsha na
wanajidanganya.
Naibu
Waziri Mpina (MB) ameyasema hayo leo
jimboni Kisesa alipokuwa katika Mkutano na Jimbo wenye lengo la kuelezea
mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utatuzi wa Changamoto za Jimbo
Hilo.
Mpina
alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano wamekuwa wakibezwa kwa kile
kinachonadaiwa wanamuogopa Mheshimiwa Rais na hawawezi kumsogelea na kumpa
ushauri.
“Naenda
kinyume na kauli hiyo kwani hao wanaosema hivyo hawaoni tunachokifanya
kuzunguka usiku na mchana kutatua kero za wananchi hii ni katika kutekeleza
azma ya chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla ya kuwafikia wanachi na
kusikiliza na matatizo yao, juzi nilikuwa Kahama, nikaenda Geita na Singida na
leo nipo Hapa Mwandoya ningefika vipi huko bila wananchi kuleta shida zao”.
Alisisita Mpina.
“Serikali
imeweza kurudisha Hekta nyingi za ardhi zilizokuwa zikimilikiwa na watu binafsi
kama Sumaye na zitarudishwa kwa wananchi, leo mnasema vipi Mawaziri wa Magufuli
hawamshauri”. Aliuliza Mpina.
Akiendelea
kuongea na wana Kisesa Mbunge wa Jimbo Hilo Naibu waziri Mpina, aliongeza kwa
kusema kuwa, Pia Ndege aina ya Bombardier
Q400 zilizonunuliwa na serikali pamoja na upanuzi wa barabara akitolea
mfano wa Barabara ya Mwenge Jijini Dar es Salaam na Barabara ya Airport ya
Mwanza, vyote vimefanyika na bado watu wanabeza bila kuona kama Mawaziri wana
Mchango na wanamsaidia Mhe. Rais Magufuli.
Akiendelea
kusikiliza changamoto za wanakisesa ikiwa ni pamoja na changamoto ya eneo la
makaburi na standi ya Mwandoya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu Bw.
Mussa Isaac Mpina alilitoea ufafanuzi na kusema kuwa jambo hilo lipo katika
mpango wa fedha wa mwaka unaokuja hivyo linasubiri utekelezaji.
Akizitaja
baadhi ya changamoto zilizotatuliwa Jimboni Kisesa ikiwa ni pamoja na Barabara,
Mitandao ya simu, upatikanaji wa maji safi na salama, na kuwepo kwa Zahanati
katika mji mdogo wa Mwandoya, Mhe Mpina alisema kuwa ndani ya muda Mfupi
zahanati hiyo itapata vifaa vya kisasa vya Ultra-Sound,
X-Ray na Fridge la kuhifadhia
Damu kwani Zahanati hiyo imeshakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji na kutoa
huduma ya uzazi.
Akiongea
kabla ya kuanza kwa Mkutano huo Diwani
wa kata ya Lugeka CHADEMA mhe.Zakayo
Sarya Maarufu kwa jina la Trump, alisema uchaguzi uliisha wakati alipotangazwa
mshindi, kazi inayofuata ni utekelezaji wa masuala ya maendeleo bila kujali
itikadi za vyama vyetu.
“
Nawashangaa sana wapinzani wenzangu wa wanaobeza mambo mazuri anayofanya Mhe,
Rais mimi Binafsi nampongeza sana kwa jitihada zake za kuleta maendeleo bila
kubagua vyama, rangi, dini wala kabila.
Awali
akihutubia Mkutano huo Naibu waziri Mpina aliwashuru wana Kisesa kwa kumuamini
na kumuweka madarakani tangu 2005
akiwa kijana mdogo na kuhaidi kuwatumikia bila ubaguzi wa aina yoyote kwa
manufaa ya taifa.
0 comments:
Post a Comment