Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje baada ya
kuwasili wilayani Mpwapwa kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia
kufanya uchaguzi mdogo Januari 22 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa
Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe baada ya kuwasili wilayani
Mpwapwa kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia kufanya uchaguzi mdogo
Januari 22 mwaka huu.Katikati ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa
Bw. Mohamed Maje.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akiongoza kikao
cha kupokea taarifa kuhusu mwenendo wa uchaguzi mdogo wa Kata ya
Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.Kulia kwake ni
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje, Mkuu wa Polisi
wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa
Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, Mkuu wa Kanda ya Kati ya
Uchaguzi Bi. Saada Kangeta na Afisa Utumishi wa Tume Athumani Masesa.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akisalimiana na Mkuu wa
Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri wakati alipomtembelea ofisini kwake
kabla ya kutembelea Kata ya Ngh’ambi.Kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi
Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la
Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (aliyesimama) akitoa maelezo ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage
(kulia kwake) baada ya kuwasili kwenye Kata ya Ngh’ambi kufuatilia
mwenendo wa uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika
Januari 22 mwaka huu.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa pili kulia) akimueleza Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (wa pili
kushoto aliyekaa) kuhusu mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata hiyo
unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari mwaka huu.Kushoto ni Mkurugenzi
wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, Msimamizi wa
Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (katikati) na kulia ni
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Clemence Fugusa.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (aliyesimama) akitoa taarifa ya mwenendo
wa Uchaguzi Mdogo wa kata hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe (kushoto) akifafanua
jambo kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa
Kata ya Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la
Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) na Mkurugenzi
wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe
baada ya kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata
ya Ngh’ambi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akikagua daftari la
kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi
kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi. Kushoto kwake aliyevaa miwani ni
Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (aliyevaa kofia nyeusi) akipokea
maelezo kuhusu mabango ya Uchaguzi kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa
Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa tatu kushoto) wakati
alipokuwa akikagua mabango hayo nje ya kituo cha kupigia kura cha Kata
ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia)
akieleza jambo baada ya kukagua mabango ya Uchaguzi kwenye kituo cha
kupigia kura cha kata ya Ngh’ambi.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za
Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe na kushoto ni Afisa Uchaguzi
halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.
Picha na Hussein Makame, NEC.
…………..
Hussein Makame, NEC-Mpwapwa
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amesema kila kitu kiko sawa
tayari kwa uchaguzi mdogo wa kumpata diwani wa kata ya Ngh’ambi iliyoko
katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mhe. Jaji (R) Kaijage
ameyasema hayo kutokana na kuridhishwa na maandalizi ya uchaguzi mdogo
wa kata ya Ngah’ambi baada ya kutembelea na kufuatilia mwenendo wa
uchaguzi wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari mwaka
huu.
Akitoa taarifa fupi ya mwenendo wa
uchaguzi mdogo wa kata hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa
Bw. Mohamed Maje alisema karibu vifaa vyote kwa ajili ya uchaguzi huo
vimepokelewa na kampeni za uchaguzi huo zinaendelea kwa amani na
utulivu.
Alisema baada ya uteuzi wa
wagombea kufanyika Desemba 22 mwaka 2016 wagombea wanne kutoka vyama vya
ADC, CCM, CHADEMA na CUF waliteuliwa ambao ni David Mazengo, Richard
Kaleme, Leornard Majenda na Hassan Kiuka, mtawalia.
Kwa upande wa pingamizi kwa
wagombea, Bw. Maje alisema walipokea pingamizi kutoka vyama vya CHADEMA
na CCM ambapo mgombea wa CHADEMA alipinga uteuzi wa mgombea wa CCM kwa
madai kuwa si mkazi wa halmashauri husika.
“Pingamizi hili lilitolewa
uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia
mbali madai hayo baada ya uthibitisho kuwa mgombea wa CCM ni mkazi
halali wa halmashauri husika.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo pia
alikubaliana na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya
kata.” alisema Bw. Maje na kuongeza kuwa:
“Mgombea wa chama cha CCM
alipinga uteuzi wa mgombea wa chama cha CHADEMA kuwa fomu ya uteuzi
namba 8 C sehemu C na D imesainiwa na mtu ambaye si Katibu wa chama
husika wa mkoa au Wilaya”
“Pingamizi hili pia lilitolewa
uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia
mbali madai hayo baada ya uthibitisho wa maandishi kuwa aliyesaini ndiye
Katibu wa chama husika wilaya ya Mpwapwa.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo
alikubaliana na uamuzi huo”
Aliongeza kuwa kamati za
maadili kwa ngazi ya jimbo na kata zinafanya kazi na kwamba hadi kufukia
Januria 13 kamati hazikupokea malalamiko yoyote kutoka kwenye vyama
vinavyoshiriki uchaguzi mdogo kata hiyo.
Alisema wanatarajia kutoa
mafunzo kwa makarani waongozaji na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura
tarehe 18 na 19 Januari na wameshaandaa vituo 12 vya kupigia kura vyenye
wapiga kura 4123.
Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la
Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe alisema hadi sasa kampeni
zinafanyika kwa kuzingatia taratibu za nchi na taratibu za uchaguzi na
hakuna vurugu zozote zilizojitokeza.
Hata hivyo aliwakumbusha
wananchi kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi na
anaamini wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa kata na kamati za maadili
zitawakumbusha wananchi jukumu hilo.
Kwa upande wa Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi Bw. James Mkinga alisema
maandalizi yote ya uchaguzi yamekamilika na wameshabandika daftari la
kudumu la wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe aliwakumbusha
wasimamizi wasaidizi kuhakikisha Sheria, kanuni na taratibu zote za
Uchaguzi zinazingatiwa.
Aliwataka wawakumbushe wananchi
kufika kwenye vituo vya kupigia kura kwa wakati ili kuepuka kukosa haki
ya kupiga kura kwa sababu ya kuchelewa kufika kituoni.
“Hakikisha mnavikumbusha vyama
vyote kuondoa mabango ya kampeni yaliyopo kituoni siku ya kupiga kura na
kama hawawezi kuyaondoa uwafahamishe kwamba utayaondoa kwa sababu
sheria inakataza” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa:
“Wakumbusheni wasimamizi wa vituo
kufuata Sheria, kanuni na taratibu na yeyote atakayekiuka Sheria Tume ya
Taifa ya Uchaguzi haitasita kumchukulia hatua za Kisheria”
Aliwakumbusha kuhakikisha kuwa
mawakala wa vyama wanafuata taratibu zote inapotokea chama kinataka
kumbadilisha wakala kwenye kituo cha kupigia kura.
Naye Mkuu wa Kanda ya Kati ya
Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Saada Kangeta
aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuwa iwapo litajitokeza jambo
linaloweza kuchelewesha matokeo kama kufanya uamuzi ya kura za mgogoro
wawafahamishe wananchi ili kuepuka vurugu.
0 comments:
Post a Comment