Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
10 February 2017
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezitaka Kampuni kubwa na za
kati kuchangamkia fursa ya uwepo wa Sekta ya Soko la Mipaji, kwa
kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es salaam ili kushiriki moja
kwa moja katika umiliki wa uchumi wa nchi.
Dkt.
Mpango ametoa rai hiyo Bungeni Mjini Dodoma, wakati akijibu swali
lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Magomeni, Mhe. Jamal Kassim Ali,
aliyetaka kujua mchango wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)
na Soko la Hisa la Dar es saam (DSE), kwa wafanyabiashara wazawa.
Alifafanua
kuwa kampuni kadhaa, ikiwemo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), TOL Gases,
Kiwanda cha Sigara (TCC), Kiwanda cha Saruji Tanga, Wakala wa Huduma za
Mizigo kwenye viwanja vya ndege-Swissport na Benki ya NMB, ni baadhi ya
kampuni zinazouza hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es salaam.
Dkt.
Mpango alisema kuwa kampuni hizo zimechangia kukuza uchumi wa nchi
ikiwemo ajira, kutoa gawiwo kwa Serikali na wanahisa, lakini pia ni
miongoni mwa walipa kodi wakubwa.
“Kwa
mfano kwa mwaka 2015 NMB, ilitoa gawiwo Serikalini kiasi cha shilingi
bilioni 16.5 na TCC shilingi billion 1.4 kwa hisa zinazomilikiwa na
Serikali huku mapato yatokanayo na kodi pamoja na gawiwo, hutumiwa
katika kutoa huduma mbalimbali ambazo jamii ikijumuisha wafanyabiashara
wadogo hunufaika nazo”alisema Dkt. Mpango
“Vilevile,
Serikali imekuwa ikitumia masoko ya mitaji kama chanzo cha upatikanaji
wa fedha za bajeti (Treasury Bonds), Miradi inayotekelezwa na fedha
hizi, pamoja na mambo mengine, imekuwa ikitoa ajira na fursa za
kibiashara kwa wafanyabiashara wazawa; wadogo na wa kati” aliongeza Dkt.
Mpango
Dkt.
Mpango, alibainisha kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa kampuni
ndogo ndogo katika kukuza uchumi wa nchi ndio maana mwaka 2013 Soko la
Hisa la Dar es Salaam lilianzisha dirisha linaloziwezesha kampuni ndogo
na za kati za wazawa zisizokidhi vigezo vya kujiunga na soko hilo
kupitia dirisha kuu, kutumia Soko la Hisa katika kupata mitaji kutoka
kwa umma wa watanzania.
Dkt.
Mpango alibainisha kuwa watanzania wengi wananufaika na uwepo wa soko
la hisa, na kushiriki moja kwa moja katika umiliki wa uchumi wa nchi
huku akizitaja baadhi ya kampuni zilizonufaika na utaratibu huo wa
dirisha dogo la hisa kuwa ni Benki ya Mwalimu Commercial
Bank, Swala Oil and Gas Tanzania, Maendeleo Bank PLC, Yetu Microfinance
na Mkombozi Commercial Bank, ambazo zina jumla ya mitaji isiyopungua
shilingi bilioni 120
0 comments:
Post a Comment