Na Nuru Juma na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka
watumishi 9932 waliogushi vyeti, kuondoka maeneo yao ya kazi haraka
iwezekanavyo kabla hawajadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akikabidhiwa taarifa
ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma sambamba na uzinduzi wa
maadhimisho ya miaka kumi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
“Watumishi
9932 wenye vyeti vya kugushi na feki mishahara yao ya mwezi huu ikatwe
na waondoke kazini mara moja na hizo nafasi zitangwazwe ili wasomi
waweze kuziomba na majina yao yawekwe kwenye magazeti ili wajulikane”
amesema Rais Magufuli
Aidha
amesema kuwa hadi kufika tarehe 15 Mei, 2017 kila mkuu wa Idara mahali
pake pa kazi ahakikishe watumishi hao wameondoka na watakao kaidi agizo
hilo amevitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia.
Hata
hivyo Rais Magufuli ameongeza kuwa watumisi 1538 wanaotumia cheti zaidi
ya mtu mmoja kutopewa mshahara hadi pale itakapojulikana nani mwenye
cheti halali na kuwataka watumishi 11,769 kuwasilisha vyeti
vilivyopungua.
Mbali
na hayo Rais Magufuli amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuachana
na masuala ya siasa kwa lengo la kujenga nchi kwani watanzania
wanahitaji maendeleo.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Angela Kairuki amesema kuwa mpaka sasa vyeti vilivyohakikiwa ni
435,000 ambapo imefanyika kwa awamu tatu iliyojumuisha Serikali za
Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya
Utumishi na Wakala wa Serikali pamoja na Serikali Kuu.
“Leo
tunakabidhi taarifa ya awamu mbili iliyohusisha Serikali za Mitaa,
Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi
na Wakala wa Serikali ambapo imejumuisha uhakiki wa vyeti vya Kidato cha
Nne, Sita, vyeti vya ualimu kwa ngazi ya cheti na stashahada” amesema
Waziri Kairuki.
Amesema
kuwa matokeo ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma yapo ya aina nne
ambapo watumishi 376,969 sawa na asilimia 94.23 wanavyeti halali,
watumishi 9932 asilimia 2.4 wanavyeti vya kugushi, watumishi 1538
asilimia 0.3 vyeti vyao vinatumika kwa zaidi ya mtu mmoja na watumishi 11,769 asilimia 2.8 wanavyeti pungufu.
Nae
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema
wizara yake inakumbana na changamoto ya watumishi wa umma kugushi vyeti
hivyo aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwani serikali imeziba njia
zote za mkato za kuajiriwa na Serikali.
“Leo
tunaandika historia ya kipekee kwani suala la uhakiki wa yveti
limefanyika kwa mara ya kwanza nchini ambapo Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ndio yenye jukumu la kuhakiki uhalali wa vyeti hivyo”
amesema Prof. Ndalichako.
Zoezi
la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma limeendeshwa na Serikali ya
Awamu ya Tano kuanzia Mwezi Oktoba, 2016 likiwa na lengo la kubaini
uhalali wa vyeti kwa watumishi wake.
0 comments:
Post a Comment