Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema inaendelea na mchakato wa
ndani wa kufanyia marekebisho ya kuhuisha na kuimarisha maeneo yaliyo
mazuri ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kuwasilishwa Bungeni ili
kuendana na wakati.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof.Palamagamba Kabudi
wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali
inaendelea na mchakato huu wa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria hii
Bungeni ili iweze kuendana na wakati kwa kuondoa upungufu uliopo kwa
maslahi mapana ya nchi yetu”,Aliongeza Mhe.Kabudi.
Amesema
kuwa baada ya miaka 20 kupita tangu sharia hiyo ya ndoa
itungwe,Serikali kupitia tume ya kurekebisha Sheria iliifanyia mapitio
ya sheria hiyo na kubaini maeneo kadhaa yenye udhaifu na hivyo kuhitaji
kufanyiwa marekebisho.
Amebainisha kuwa Kutokana na maoni hayo ya tume,mwaka 2008 Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria iliandaa waraka wa
baraza la Mawaziri uliokuwa na mapendekezo ya marekebisho ya sharia ya
ndoa ya mwaka 1971,hata hivyo desemba 2010 kabla waraka huo kujadiliwa
na kuridhiwa na baraza la Mawaziri mchakato wa mabadiliko ya katiba ya
jamhuri ya muungano ukaanza na kulilazimu Baraza kusitisha kwa muda
mchakato huo.
“Serikali
ilikuwa na matarajio kuwa wakati tume ya mabadiliko ya katiba
inakusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba,wananchi
wangetoa maoni kuhusu Sheria ya ndoa pamoja na sheria nyingine zinazofanana na hiyo na hivyo maoni yaliyotolewa wakati wa Sheria ya Ndoa yalikuwa machache sana”Alifafanua Mhe.Kabudi.
Sheria ya ndoa mwaka 1971 ni matokeo ya mjadala mpana na shirikishi kupitia waraka wa Serikali namba moja wa mwaka 1969.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment