Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) kwa kushirikiana
na wadau iko katika hatua za mwisho kukamilisha Mkakati wa Taifa wa
miaka mitano wa kupanda na kutunza Miti nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira)Mhe.Luhaga Mpina wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo
Mjini Dodoma.
“Tunaitaji kiasi cha shilingi bilioni 105 ambapo kila mwaka tutatenga bilioni
20 kutoka vyanzo mbalimbali vya Serikali na wadau wa maendeleo kwa
ajili ya utekelezaji wa mkakati huu ambao unaelekeza kila
mwananchi,Taasisi za Serikali,Taasisi za madhehebu,Asasi zisizokuwa za
Serikali,kambi za Majeshi,Magereza,Shule na makampuni kupanda na kutunza
miti katika maeneo yao”,Alisema Mhe.Mpina.
Aidha
amesema kuwa mkakati huu ni tofauti na mikakati mingine iliyopita kwani
kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini itahakikisha kwamba miti
inayopandwa inatunzwa na kukua na kuhakikishia visababishi
vinavyochangia miti kutokuwa vimebainishwa na mikakati ya kuvidhibiti
imeandaliwa ikiwa ni pamoja na upandaji wa aina ya miti kulingana na maeneo na utunzanji wa miti hiyo.
Hata
hivyo Serikali imekuwa ikitekeleza zoezi la upandaji miti kote nchini
kupitia Ofisi hii ambapo kila halmshauri inatakiwa kupanda miti
1,500,000 kila mwaka na kuhakikisha inatunzwa nna pale itakapoonekana
inafaa Halmshauri zihahakishe maeneo ya wazi yanahifadhiwa ili kuruhusu
uoto wa asili kurejea.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment