Na Daudi Manongi-MAELEZO DODOMA.
Serikali imesema kuwa inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya Tumbaku kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Tumbaku nchini.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini
Dodoma.
“Serikali
ilivunja Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji
kazi wa Bodi,na hatua hii ya kuvunja Bodi ya wakurugenzi haihusu
kusitisha shughuli zinazotekelezwa katika sekta hii ya tumbaku kwani
wapo wataalamu wanaoendeleza utekelezaji wa mpango uliopo wa kuendeleza
zao la tumbaku”. Aliongeza Mhe.Ole Nasha.
Aidha
amesisitiza kuwa upatikanaji wa pembejeo za zao hilo zitapatikana
kupitia vyama vikuu vya ushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa
zabuni unaosimamiwa na kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.
Amezitaja
pembejeo za muhimu kwenye zao la tumbaku kuwa ni mbolea aina ya NPK,
Mbolea aina ya CAN, nyuzi za kufungia tumbaku wakati wa kuvuna na wakati
wa masoko zote zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika.
Ameeleza kuwa kwa kuzingatia kuwa wakulima wanahitaji huduma muhimu hasa
katika kipindi hiki cha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa
2017/18, Serikali imeateua timu kwa ajili ya uratibu na kusimamia
masuala hayo.
“Tuna
timu tayari iko mkoani Tabora ambayo itasimamia na kuratibu masuala
mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wa
pembejeo kwa msimu ujao,hivyo pamoja na WETCU kuvunjwa kazi za chama
hicho zinaendelea kama kawaida”Alisema Mhe.Ole Nasha.
0 comments:
Post a Comment