Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa Rasimu ya
Muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizi na
udhibiti wa bishara ya chuma chakavu katika hatua mbalimbali za
uzalishaji, ukusanyaji, usambazaji, uuzaji na uyeyushaji wake kwa
kuzingatia uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa manufaa ya Taifa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles
Mwijage wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Biashara
ya Chuma chakavu imeshamiri hapa nchini na duniani kwa ujumla,na hili
limetokana na mahitaji ya vyuma chakavu ambapo kumetumiwa na wahalifu
kuaharibu miundombinu iliyojengwa kwa vyuma kwa nia ya kupata chuma ili
waiuze kama chuma chakavu”Alisema Mwijage.
Amesema ili kukabiliana na hujuma hizi Mamlaka husika zikiwemo TANESCO, TANROADS na RAHACO
wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na jeshi la Polisi ikiwemo kutumia
walinzi wa Taasisi husika ili kulinda rasilimali hizo.
Amesisitiza kuwa Muswada huu umeweka wazi na bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu atakayebainika kuharibu miundombinu.
Aidha Mhe.Mwijage ametoa wito kwa watanzania kutoa taarifa pindi waonapo mtu anayehujumu miundombinu kwa namna yote ile.
“Natoa wito kwa wenye viwanda na wafanyabiashara wa vyuma chakavu jiepusheni na ununuzi wa vyuma ambavyo asili yake ina mashaka na tutaharakisha sheria hii ili kutatua tatizo hili”Aliongeza Mwijage.
0 comments:
Post a Comment