Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini zaridhia kutekeleza
Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
Makubaliano
hayo yamefanyika tarehe 19/09/2017 baina ya Tanzania na Afrika Kusini
yakiwahusisha Mawaziri wenye dhamana ya Utamaduni kutoka nchi hizo
pamoja na Mawaziri kutoka Wizara za kisekta zinazohusika na utekelezaji
wa Programu hiyo.
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema
kuwa Tanzania ina mchango wa hali na mali katika harakati za ukombozi
wa nchi za Bara la Afrika pamoja na uanzishwaji wa program hiyo
inayolenga kuhifadhi Urithi huo kwa kushirikiana na wadau.
“ Mwaka 2002
programu hiyo iliridhiwa na Mkutano Mkuu wa 33 wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Mkutano Mkuu wa Umoja
wa Afrika (AU) wa mwezi Januari, 2011” ameongeza Dkt. Mwakyembe.
Aidha,
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa, moja ya makubalino ni kuendeleza jitihada
za kufanya tafiti zaidi baada ya kukamilika kwa utafiti wa Mradi wa
Hashimu Mbita na kufanya juhudi za makusudi kuorodhesha nyaraka za
iliyokuwa Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika katika kumbukumbu ya
Dunia.
Kwa
upande wake Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini Nathi
Mthethwa amesema kuwa Programu hiyo itaimarisha ushirikiano katika
kuongeza idadi ya maeneo ya Urithi wa Dunia yanayohusiana na Harakati za
Ukombozi yanaorodheshwa kwa pamoja baia ya nchi moja na nyingine
hususani Urithi wa Ukombozi usioshikika.
“Kuna
baadhi ya vizazi havielewi machungu ya kutawaliwa, hivyo nashauri
mifumo ya elimu katika nchi za Afrika izingatie masuala ya ukombozi wa
Bara la Afrika ili kuleta uelewa kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo”
ameongeza Mhe. Mthethwa.
Programu
hiyo ina wajibu wa kukusanya, kuweka kumbukumbu, kuhifadhi na kukumbuka
nakishi ya Urithi wa Afrika tangu harakati za kupigania Uhuru wa Afrika
hadi Bara zima lilipokombolewa.
0 comments:
Post a Comment