Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi.
Khadija Mwenda akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati
wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi
Leo Mjini Dodoma.Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw.
Eric Shitindi akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati
wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi
ambapo aliwashauri wafanyakazi nchini kupima afya mara wanapostaafu ili
kujihakikishia kama hawajaathirika na kazi walizokuwa wanafanya.Katikati
ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)
Bw.Qambos Sule na Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na
Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda
Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule
akiongea naViongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi
wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi, kulia ni
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
Bw. Eric Shitindi na kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama
na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda
Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule
(KUSHOTO) na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.
Jones Majura(KULIA) wakiteta jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri
Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi baada ya
ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi leo
Mjini Dodoma
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw.
Eric Shitindi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Semina kuhusu
masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma. PICHA NA
IDARA YA HABARI-MAELEZO,DODOMA
Na: Lilian Lundo – MAELEZO Dodoma.
Wafanyakazi
nchini wameshauriwa kupima afya zao mara tu wanapostaafu ili
kujihakikishia ikiwa hawajaathirika na kazi ambazo wamekuwa wakizifanya.
Hayo
yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu Eric Shitindi alipokuwa akifungua semina ya viongozi wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na viongozi wa
Vyama vya Wafanyakazi juu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, leo Mjini
Dodoma.
“Kumekuwa
na mazoea kwa wafanyakazi kupima Afya pale tu wanapoajiriwa na
kutotilia maanani upimaji afya zao mara wanapostaafu ili kujua ikiwa
kazi wanazozifanya zimewaathiri kwa kiasi gani,” amesema Shitindi.
Ameendelea
kwa kusema kuwa, upimaji wa afya mara baada ya kustaafu utasaidia
watumishi kujua afya zao na ikiwa watakuwa wameathirika upitia kazi
walizokuwa wakizifanya basi mwajiri atawajibika mkulipa fidia mtumishi
huyo.
Aidha
amesema kuwa licha ya juhudi za Serikali katika kusimamia Usalama na
Afya maeneo mengi ya kazi sio ya kuridhisha kutokana na waajiri wengi
kutokuzingatia sheria na kanuni mbalimbaliza Usalama na Afya.
Hivyo
basi kutokana na waajiri hao kutofuata sheria na kanuni hizo
kumesababisha maeneo mengi ya kazi kulalamikiwa kutokana na ukiukwaji wa
sheria hizo.
Vile
vile amesema kuwa baadhi ya waajiri na wafanyakazi wana uelewa mdogo
kuhusu kuzingatia maelekezo ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ikiwemo
matumizi sahihi ya vifaa kinga.
Kwa
upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa
Kazi (OSHA) Khadija Mwenda amesema kuwa, wameamua kuandaa semina hiyo
kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi hapa nchini ili na wao wakatoe
elimu hiyo kwa wafanyakazi wote nchini kutokana na wafanyakazi hao
kutokuwa na uelewa mzuri juu ya masuala ya Usalama na Afya Mahali pa
Kazi.
0 comments:
Post a Comment