BUNGE limeweka wazi kuwa hawatambui wanachama wanane waliovuliwa
uanachama na Chama cha Wananchi (CUF) na baadaye kutangazwa kuvuliwa
nafasi zao za ubunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Taarifa hiyo ya Bunge, imetokana na barua ya CUF kwenda kwa Katibu wa
Bunge, Stephen Kigaigai inayomtaka amjulishe Spika wa Bunge hilo, Job
Ndugai, kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu ya kutengua uamuzi wa awali wa
chama hicho wa kuwafuta uanachama wa wabunge hao na kuomba Bunge
liwatambue kama bado ni wabunge halali.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hiyo ya Mahakama Kuu
kutengua uamuzi wa awali wa CUF wa kuwafukuza uanachama wabunge hao,
Kigaigai alikiri kupokea barua ya chama hicho, lakini alisisitiza kuwa
bado chombo hicho hakiwatambui kama wabunge halali.
“Ndio nimeipata barua yao na naanza kuifanyia kazi, ila kifupi tu
Bunge haliwatambui watu hao. Sisi tunawatambua wabunge wapya tuliopatiwa
orodha na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),” alisisitiza.
Alisema kwa kawaida Bunge hupokea majina ya wabunge wote, wanaoingia
ndani ya chombo hicho kutoka NEC na si kwa chama husika, hivyo mpaka
sasa hawajapata barua yeyote kutoka kwa tume hiyo, inayobainisha uhalali
wa watu hao kuwa wabunge.
Wanachama hao waliokuwa wabunge wa viti maalumu, baada ya kuvuliwa
uanachama wao Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba
kutokana na ukosefu wa nidhamu, walikosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Wanachama hao ni Saumu Heri Sakala, Salma Mohamed Mwassa, Raisa
Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Khadija Salum Ally Al-Qassmy na Halima
Ali Mohamed. Baada ya kuvuliwa uanachama na kuvuliwa ubunge, NEC
ilitangaza majina ya wabunge wapya waliochukua nafasi za wabunge, ambao
tayari waliapishwa na wanaendelea kulitumikia Bunge hilo.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment